
Bible Lessons
for
THE CHURCH OF ELOHIM
(7th Day)
__________
FIRST QUARTER
2019
_____________
FOR
JANUARY - FEBRUARY - MARCH
TO BE USED WITH THE BIBLE
____________
Workers are needed, for the harvest
is great, but laborers are few ...
Address all orders to P.O. Box 568,
Jerusalem - Israel
---------------------------------------------------------
Lesson for January 5, 2019
LAST DAY CONDITIONS PRE-ANNOUNCED
Scripture reading: 2 Tim. 3rd chapter.
Memory verse: 2 Tim. 3:14.
1. Describe the perilous times of which Paul spoke and tell when will they take place? 2 Tim. 3:1-7.
2. What did Paul mean in verse 7?
3. Will there a time come when there will be fewer seducers? Verse 13.
4. For what purpose did Paul say that these scriptures were written? Verses 16-17.
5. What will some of the people who think they are the children of Elohim be doing in the last days? 1 Tim. 4:1.
6. What will they be saying, and why? 1 Tim. 4:2.
7. What will be the condition of the rich people in the last days? James 5:1-3.
8. Besides living in pleasure, what have they done? Verse 6.
9. What did Paul tell the faithful brethren to do? Verses 7-13.
10. In these times of peril, what did Yahshua say we should take heed to? Luke 21:34, 35.
11. What was Paul’s instruction to the Church for these last days? Heb. 10:25.
12. How will the worldly people act when the Son of man is revealed coming down from Heaven and all the mighty angels with Him Rev. 6:12-17; Matt. 24:30.
Note. — It is evident from all the signs about us that we are living in the last days. Perilous times are here, and it behooves every one of us to lift up our heads for our redemption draweth nigh. — Luke 21:28. Also to be about our Father’s business, as profitable servants of the Lord. --- Matt: 24:19-30.
*******************************
Lesson for January 12, 2019
REMOVE NOT THE ANCIENT LANDMARKS
The “ancient landmarks” depicts the old faith which was delivered unto the Saints — (Jude 3). The foundation was laid by the Apostles and Prophets, the foundation stone being Yahshua Messiah. To be against Yahshua means to be against His life and His teachings.
It should be explicitly known to everyone that the church of Elohim — Elohim’s family on earth — does not have a "closed and stamped creed”. Since Elohim is an Omniscient Being, His knowledge and wisdom is worldwide and unconfined. It is revealed and magnified in the hearts of true Messianics, from age to age and from generation to generation.
Scripture Reading: 2nd John.
Memory Verse: Prov. 22:28.
1. Upon what is the Messianic’s foundation built? Eph. 2:20.
2. Should this originally-laid foundation be remodeled and renovated? 1 Cor. 3:10-15.
3. What are some of the given conditions by which this foundation was laid? Rev. 14:12, 12:17; Luke 9:23-26.
4. How was Moses cautioned concerning the building of Elohim’s Tabernacle? Ex. 25:8-9, 40; Heb. 8:5.
5. What will be the conditions of Messianics if the ancient landmarks are destroyed? Ps. 11:3, 82:5.
6. What are Messianics admonished to earnestly contend for? Jude 3.
7. What is prophesied concerning some Messianics departing from the true faith? 1Tim. 4:1-3.
8. What are those false teachers likened to? Should one keep company with them? 1 Tim. 6:3-5; 2 John 9-11.
9. How can one detect a false Messianic or anti-Messiah? Luke 9:49-50; John 7:17; 1 John 4:1-3.
10. During the days of the early Messianics, how did certain men endeavor to destroy the ancient landmarks? Acts. 15:1,5.
11. When the wise elders of the church investigated the truth about the matter, what did they do? Vs. 2, 4, 6.
12. In the emergency meeting held, what resolution did they undertake? Vs. 23-29.
13. What is Paul’s counsel to the remnant people who are earnestly contending for the old faith delivered unto the saints? 1 Cor. 1:10.
14. Why was Titus left in Crete? Titus 1:5.
15. What is the fate of those who deliberately digress from the teachings of the Gospel? Gal. 1:6-9; Rom. 16:17-18; 2 Thess. 3:6.
*******************************
Lesson for January 19, 2019
GRACE – ELOHIM’S GREATEST GIFT
Scripture reading: Romans 5:1-21.
Memory verse: Romans 5:21.
1. What is the first recorded act of grace towards fallen man? Genesis 3:21.
Note: The awfulness of sin and its consequences; death to the innocent party, is told in this short verse. Innocent blood shed that man might receive physical covering. Thus the first type was formed in the Old Testament. It pointed forward to the shed blood which would cover the spiritual man as completely as their first needs were met.
2. How do we know that Abel was instructed regarding the plan of salvation? Gen. 4:4.
3. What is the relationship between sin and grace? Romans 5:17-20.
Note: Just as surely as sin and death came through the fall of man, so much more are we assured it will pass away because of the death and resurrection of Yahshua the Son of Elohim.
4. Even in ancient times, what two ways were open to man? Deut. 30:19; Jer. 21:8.
5. How did Yahshua express the same thought to the Jews? John 5:40.
6. what message of grace should we be heralding today? Rev. 22:17.
Note: Down through the ages Elohim has been extending His grace to the human race. Age after age tending His grace to the human race. Age after age they rejected His mercy and love until at last they crucified the very Son Himself. The closer we get to the second coming the more noticeable will be the rejection of the sacrifice He made. Yet to those who know Him, He is still as real as when He walked on this earth.
7. To how many has the grace of Elohim appeared? Titus 2:11-15.
8. What shows the immeasurable love Messiah has for us? 2 Cor. 8:9.
9. How is grace further extended to us? Verse 12.
10. What humble confession did Paul make? 1 Cor. 15:10.
11. How did he express grace for the past, present, and future? 2 Cor. 1:10.
12. In accepting Messiah what is it possible to know? Acts 13:38, 39.
*******************************
Lesson for January 26, 2019
ELOHIM’S POWER OF DELIVERANCE
Scripture reading: Isaiah 54:4-17.
Memory verse: Psalms 103:17.
1. When the priests’ feet touched the water, what happened to the river Jordan? Joshua 3:15, 16.
2. Where were the priests while the children of Israel passed over the Jordan river? Verse 17.
3. What were the twelve men, one of each tribe, commanded to do? Joshua 4:5.
4. What were the stones to represent and what were the children of Israel commanded to do with them? Verse 6-8.
5. Where did Joshua finally place the stones? Verse 9.
6. How did the children of Israel pass over Jordan? Verse 10.
7. When and how did the ark of the Lord, and the priests, pass over Jordan? Verse 11.
8. What did Joshua say that all the people of the earth might know? Verse 24.
9. How were the three Hebrew children delivered from the fiery furnace? Daniel 3:24-27.
10. In what way were the lion’s mouths shut, that they could not destroy Elohim’s faithful servant, Daniel? Daniel 6:16, 19-23.
11. In what miraculous way were Paul and Silas delivered from prison? Acts 16:25, 26.
Note: What a wonderful, loving, all-powerful Heavenly Father we are privileged to serve and depend upon for our very existence! He is not willing that any should perish, but all should come to Him and be saved. Let us strive to know and to do His will and help others to come to the light of the gospel of Messiah and its fullness, and be saved.
*******************************
Lesson for February 1, 2019
IMMERSION, ELOHIM’S MODE OF BAPTISM
Scripture Reading: Matthew 3.
Memory verse: Colossians 2:12
1. The baptism of Jesus, how and by whom was it performed? Matthew 3:13-16.
2. What does the apostle Paul have to say with reference to the mode of baptism in his day? Colossians 2:12.
3. After Paul and Silas were miraculously released from prison, what very important person and family were converted and baptized? Acts 16:29-33.
4. How should we walk after we are baptized, or buried with Him in baptism? Romans 6:4.
5. How do we put on Messiah? Galatians 3:27.
6. Are we by immersion baptized into Messiah’s death? Romans 6:3-4.
7. By whom, and in what way, was the converted eunuch baptized? Acts 8:38.
8. How many modes of baptism are there? Ephesians 4:5.
9. Were there many converted and baptized after hearing Peter’s sermon on the day of Pentecost? Acts 2:41.
10. Were there others who believed and were baptized after hearing Philip’s preaching concerning the kingdom of Elohim and Yahshua Messiah? Acts 8:12.
11. Why did John baptize in Aenon? John 3:23.
Note. The above verses substantiate the fact that immersion is the right mode of baptism. If sprinkling is sufficient, why should John want so much water for baptizing? Sprinkling is erroneous, and is a very sad situation that so many have been deceived by such doctrine and still want to hold on to it. Let us pray that they may see the true light and accept true light and accept Elohim’s plan of salvation in its fullness.
*******************************
Lesson for February 9, 2019
DIVINE VIRTUE THROUGH THE HOLY SPIRIT
Scripture reading: Philippians 2:1-28.
Memory verse: Philippians 2:15.
Note. — This wonderful chapter teaches us how to get along with others in true harmony and happiness. Note these words: “If there be any consolation in Messiah, if comfort of love, if fellowship of the Spirit”, etc.
1. What four things are necessary to attain this unity as given in Philippians. 2:2?
2. Instead of working through strife and vain glory, how should we perform our works? Verse 3.
Note. How beautiful are the words, “in lowliness of mind let each esteem others better than themselves.”! If we consistently follow this excellent advice, there can be no strife. How could there be?
3. What marvelous attainment will result from this practice? Verses 4, 5.
4. Did Messiah Yahshua exalt Himself in any, manner? Verse 8.
5. What followed His great humility? Verses 9-11.
6. If we can be blameless in our dealings with one another, what will result in our cases? Verses 14, 15.
7. What happy state existed among the Brethren in the days of Paul? Verses 18-20.
8. What similar admonitions are given in Colossians 3:11-17?
9. When Messiah dwells within us by the Holy Spirit, what is always the result? John 15:4, 5.
10. If we do not sacrifice to win souls for the Kingdom of Elohim, what is always the result? Verse 6.
11. Will soul winning increase our power with Elohim in answered prayer? Verses 7, 8, 16.
*******************************
Lesson for February 16, 2019
FAITHFUL STEWARDSHIP DOCTRINALLY
Scripture reading: Titus 1:1-15.
Memory verse: Titus 2:1.
1. What did the apostle Jude say we should earnestly contend for? Jude 3.
2. What two kinds of doctrine are there in the world? Matt. 7:28, 29; 1 Tim. 4:1.
Note. — In these two texts are mentioned the doctrines of Messiah, and the doctrines of devils.
3. What is the doctrine of Messiah according to 1 Tim 6:3-5?
4. What did Yahshua say of His doctrine? John 7:16.
5. Why did He say this? John 6:38; 5:30.
6. How and through what medium can we know the true doctrine? 2 Tim. 3:16, 17.
7. Through what medium does the Holy Spirit work to reveal the wonderful saving truth? 2 Pet. 1:20, 21; Heb. 10:25; Rev. 2:7.
8. Will obedience to sound doctrine help us? Rom 6:17, 18.
9. As children of Elohim and teachers, what are we commanded to teach? Titus 2:1.
10. Should sound doctrine condemn all manner of sin? What is sin? 1 Tim. 1:9-10.
11. By sound doctrine what may we be able to do? Titus 1:9.
12. If we give heed to true Bible doctrine, what will it do? 1 Tim 4:16.
13. What did Messiah Yahshua command us not to leave undone? Matt. 23:23.
14. Why were the people astonished at the doctrine of Messiah? Matt. 7:28, 29.
Note. — Messiah spake with authority because He taught the Word in its purity, and no opponent relying upon false doctrine was able to successfully resist it; so it is with everyone today who is able to take the unadulterated Word as their guide.
15. How did Paul say some would regard sound doctrine in times to come? 1 Tim. 4:1-4.
*******************************
Lesson for February 23, 2019
LOVING ONE ANOTHER
Scripture reading: John 14:15-31.
Memory verse: John 14:21.
1. What is one of the attributes of Elohim? 1 John 4:8, 16.
2. How did Elohim reveal His love to the world? John 3:16; Romans 5:8; Ephesians 2:4,5.
3. What is required of everyone who accepts Messiah as their personal Saviour? John 13:34; 15:9, 10, 12.
4. How may the world know that we are followers of Messiah Yahshua? John 13:35.
5. Through what agency do we receive this love? Romans 5:5.
6. What is the only thing we are admonished to owe any man? Romans 13:8 (first part).
7. What do we do when we love one another? Verse 8 (last part).
8. How did our Lord emphasize this same truth? Matthew 22:34-40.
9. How do we approve our love for one another? Galatians 5:14,15.
Note: On our love to Elohim, and our fellow man, hang all the law and the prophets. If we harm our brother through gossip it is evident that the love which Elohim shed in our hearts has leaked out to some extent, for love worketh no ill to his neighbor.
10. How did Yahshua emphasize the greatness of His love for us? John 15:13.
11. How has the Lord commanded us to love one another? Verse 12.
12. What will this love cause us to put on? Colossians 3:12.
*******************************
Lesson for March 2, 2019
HUMILITY VERSUS PRIDE
Scripture reading: Daniel 4:19-37.
Memory verse: Proverbs 16:19.
1. What are some of the things Solomon said would come as a result of pride? Proverbs 11:2; 13:10
2. How are pride and humility contrasted? Proverbs 29:23.
3. What did David say about pride? Psalms 10:2; 12:3,4; 73:3-6.
4. What happened to Pharaoh because of his pride? Exodus 5:2; 14:8,28.
5. What did pride cause King Uzziah to do, and what was the final result? 2 Chronicles 26: 16, 19, 21.
6. Why was wrath pronounced upon Israel during Hezekiah’s reign? 2 Chronicles 32:24-26.
7. What lesson of humility did Yahshua teach? Luke 14: 7-11.
8. What exhortation of humility did Paul give? Romans 12:3; 11:18-21.
9. With whom did the prophet Isaiah say the Holy One would dwell? Isaiah 57:15.
10. What is necessary for sinners to do in order to become children of Elohim? Matthew 18:3,4; James 4:10.
11. What act of of humility did Yahshua display shortly before His crucifixion? John 13:3-5.
12. What severe punishment was meted out to King Herod because he did not give Elohim glory? Acts 12:21-23.
13. What admonition does Yahshua give to the proud? Revelation 3:17,18.
Note: It has been said: “The tongue gets us into trouble and pride keeps us there.” Let that not be true of Elohim’s children. May we always remember the words of Solomon “With the lowly there is wisdom.” Proverbs 11:2.
*******************************
Lesson for March 9, 2019
KEEPING OUR CONVERSATION ARIGHT
Scripture Reading: James 3rd Chapter
Memory Verse: Psalms 50:23.
1. How important are our words? St. Matthew 12:37.
2. From what source do our words come? St. Matthew 12:34, 35.
3. What was King David’s prayer concerning the meditations of his heart and the words of his mouth? Psalms 19:14.
4. What does the ninth commandment forbid? Ex. 20:16.
5. In what way did the Lord Elohim admonish the Children of Israel about the tongue? Leviticus 19:16.
6. Unto what are the words of a talebearer likened? Proverb 26:21-22; 17:9.
7. What effect will restraining from tale bearing have upon a strife torn people? Proverbs 26:20.
8. What did Solomon, the wise man, say about words that are fitly (wisely) spoken? Proverbs 25:11.
9. How vast is the difference in the speech from the lips which are controlled by the Lord and those which are not? Isaiah 57:19-21.
10. What is one called who can control his tongue? James 3:2.
11. Why must Messianics be so very careful about their speech? St. Matthew 12:36, 37.
12. Does the Lord our Elohim know all about words? Psalms 139:4.
Note. — One thing which seems so easy and natural for many people to do is to talk foolishly. There are too many things to say that will amuse people and make them laugh. This is one of the chief enjoyments of worldly people, but Messianic have a higher and greater joy than this, and it is out of place for them to make practice of such foolishness.
13. Along with what other base sins is foolish talking likened? Ephesians 5:3, 4.
*******************************
Lesson for March 16, 2019
THE GOOD AND THE BAD FIGS
Scripture reading: Jeremiah 24.
Memory verse: Jeremiah 24:7.
1. Of what are the good figs a type? Jer. 24:5-6.
2. Were the good figs to receive better treatment than the vile ones? Verse 7.
3. What portion of Judah was represented by the vile figs? Verse 8.
4. How were the vile figs to be punished, and would any be left? Verse 9 and 10.
Note: From the forgoing scripture it is very plain that there were two different classes of the Jews that into the exile, and promises were different to each class. He is still able to separate the good from the bad, just as was done back there and He is doing the same today.
5. What class of Jews was to be selected to build the waste cities and do the very work that we see going on here now? Jeremiah 24:1-7.
6. How many blows were struck in destroying the kingdom of Judah? Ezekiel 21: 25-27. Compare 2 Chronicles 36:15-19.
Note: It is said of the gentile enemies of Israel: “As thou hast done it shall be done into thee.” - Obadiah 1:15; Joel says: “I will return your recompense upon your own head.” - Joel 3:7.
7. In this destruction of the kingdom of Israel 2,500 years ago, were those represented by the evil figs taken away first or last? Compare Jer. 24:8 with 2 Chronicles 36:11,12,16.
Note: Zedekiah and his princes were the evil figs, and they were left, while the good figs were removed, just as it is going to be in the end, the good will be taken first.
8. When were the good figs, including Daniel and his companions, and many others taken away? Daniel 1:1-6.
Note: They were removed with King Jehoiakim and not left at Jerusalem when the terrible destruction came in which men, women and children were given to the sword alike.
9. What especially is said of Daniel concerning his conduct and diet? Daniel 1:7-8.
10. Before the great destruction of the wicked at the end of the gentile period, will the righteous be gathered first? Revelation 14:18.
11. After the cluster of the fruit is gathered then what happens to the wicked compared to the vine of the earth? Verse 19 and 20.
12. Where are we told the righteous will be, who have the victory over the beast and his image, when the plagues fall? Revelation 15:1-6.
Note: Notice particularly that verse 5 says: “After this”, that is, after the saints were seen in this place which appeared like a sea of glass to the prophet, he saw the angels come forth with the seven last plagues – Verse 6. Notice also that the battle of Armageddon comes at the time of the 6th plague. - Rev 16:12-15. Hence the righteous are seen assembled somewhere in deliverance from these plagues. Nothing is said where this place is, neither does it say they were caught up as we hear it so often quoted.
*******************************
Lesson for March 23, 2019
THE CONCEPTION AND BIRTH OF YAHSHUA
Scripture reading: Matthew 1:16-25.
Memory verse Matthew 1:18.
1. What message did the angel give to Mary? Luke 1:28-31.
2. Was Mary surprised at what the angel told her? Luke 1:34; Matt. 1:18.
Note. — The Holy Scriptures tell us that Mary was a chaste virgin that she knew not a man. She was engaged to be married to Joseph, but before he knew her as his wife, she was with child by the Holy Ghost. Matt. 1:18-20; Luke 1:35.
3. What was the relationship between Joseph and Mary before the birth of Jesus? What was the source of Messiah’s conception? Matt. 1:18; Luke 1:35.
4. What did Isaiah prophesy about this wonderful event? Isa. 7:14; compare with Matt. 1:23; Luke 1:31.
5. What did Joseph intend to do? Matt. 1:19.
6. What did the angel of the Lord make known unto Joseph in a dream? Matt. 1:18-25.
7. When Joseph and Mary arrived at Bethlehem how welcome were they? Luke 2:4-8.
8. What name was given to the child by the angel even before he was conceived? Matt. 1:25.
9. How is the importance of this name emphasized? Acts 4:10-12: Phil. 2:9-11.
10. What does Paul say about the fulfillment of this? 1 Tim. 3:16.
Note. — This prophecy and its fulfillment has been the target of infidels and modernist for centuries. Here the power of Elohim was manifested by the miraculous conception and birth of his dear Son, Jesus. Again and again, Yahshua told His listener that He came down from above and that Elohim was His Father.
11. What happened while the shepherds were keeping watch over their flocks? Luke 2:8-14.
12. What experience did they have with the angels? How did this effect them? Luke 2:9.
13. What sign was given to them regarding this child? Luke 2:12.
14. What glorious scene were the shepherds allowed to witness? Luke 2:13-14.
15. How did the angels express their joy at this time, for what had taken place? Luke 2:14.
16. How did the shepherds respond to this announcement? Luke 2:16-20. Should this be an example for us? Isaiah 12.
*******************************
Lesson for March 30, 2019
MESSIAH’S PRAYER TO BE GLORIFIED
Scripture reading: John 17.
Memory verse: John 17:5.
1. For what did Messiah Yahshua pray to the Heavenly Father? John 17:1.
2. What power has been given to Messiah by the Father? John 17:2.
3. What is life eternal? Verse 3.
4. In what way had Messiah glorified the Father? Verse 4.
5. How did Messiah continue to pray to the Father? Verse 5.
6. What had Messiah manifested to the men which His Father had given Him? Verse 6.
7. What other very important and necessary thing did He bring them from the Father? Verse 8 (first part).
8. Had they believed and received Him? Verse 8 (last part).
9. Did He pray alone? Verse 9.
10. In His prayer to the Father, for them, what did He ask Him to do? Verse 11.
11. How were His followers kept while He was in the world? Verse 12.
12. What attitude did the world have towards them? Verse 14.
*******************************
Bible Lessons
for
THE CHURCH OF ELOHIM
(7th Day)
__________
FIRST QUARTER
2019
_____________
FOR
JANUARY - FEBRUARY - MARCH
TO BE USED WITH THE BIBLE
____________
Workers are needed, for the harvest
is great, but laborers are few ...
Address all orders to P.O. Box 568,
Jerusalem - Israel
---------------------------------------------------------
Kiswahili
(Tevet 28, 5779)
HALI YA SIKU ZA MWISHO KUTABIRIWA
Somo Kuu: 2 Tim. 3.
Fungu La Kukariri: 2 Tim.3:14.
1. Elezea kuhusu nyakati za hatari ambazo Paulo alinena na ni lini zitatukia? 2 Tim.3: 1-7.
2. Paulo alimaanisha nini katika aya ya 7?
3. Je, Kuna wakati unakuja ambapo kutakuwa na watu wachache ambao ni wadanganyaji? Mst wa 13.
4. Ni kwa manufaa gani Paulo alisema kwamba maandiko haya yaliandikwa? Mstari wa 16-17.
5. Je, Watu wengine wanaofikiria kuwa ni wana wa Elohim watakuwa wakifanya nini siku za mwisho? 1 Tim.4: 1.
6. Watakuwa wakisema nini, na ni kwa nini? 1 Tim.4: 2.
7. Ni nini itakuwa hali ya watu matajiri katika siku za mwisho? Yakobo 5: 1-3.
8. Kando na kuishi katika anasa, wao walifanya nini? Mstari wa 6.
9. Yakobo aliwaambia ndugu ambao ni waaminifu wafanye nini?Mstari wa 7-13.
10. Katika nyakati hizi za hatari, Yahshua alisema ni nini tunapaswa kuangalia? Luka 21:34, 35.
11. Je, ni maagizo gani Paulo alitoa kwa Kanisa katika siku hizi za mwisho? Waebr.10:25
12. Watu wa dunia watafanyaje wakati Mwana wa Adamu atakapofunuliwa akishuka kutoka Mbinguni pamoja na malaika wote wenye nguvu pamoja naye Ufunuo 6: 12-17; Mat. 24:30.
Fahamu: Ni wazi kutokana ishara zote zinazotuhusu kwamba tunaishi katika siku za mwisho. Nyakati za hatari ziko hapa, na ni lazima tuinue vichwa vyetu kwa sababu ukombozi wetu unakaribia. - Luka 21:28. Pia kufanya kazi ya Baba yetu, kama watumishi wenye faida kwa Bwana. — Mat: 24: 19-30.
*********************
(Shevat 6, 5779)
USIONDOE ALAMA YA MPAKA WA ZAMANI
“Alama za kale” zinaonyesha imani ya zamani ambayo ilikabidhiwa Watakatifu - (Yuda 3). Msingi uliwekwa na
Mitume na Manabii, jiwe la msingi ni Yahshua Masihi. Kuwa kinyume cha Yahshua inamaanisha kuwa kinyume na maisha yake na mafundisho yake. Inapaswa kuwa wazi kwa kila mtu kwamba kanisa la
Elohim - familia ya Elohim duniani - haina”imani iliyofungwa na kutiwa mhuri.” Kwa kuwa Elohim
anajua mambo yote, ujuzi na hekima yake imejaa duniani kote na haichunguziki. Imedhihirishwa katika
mioyo ya WaMasihi wa kweli, kwa nyakati zote na kutoka kizazi hadi kizazi.
Somo Kuu: 2 Yohana.
Fungu La Kukariri: Mithali. 22:28.
1. Msingi wa uMasihi umejengwa juu ya nini? Waefeso. 2:20.
2. Je, Msingi huu uliowekwa awali unapaswa kubadilishwa na kurekebishwa? 1 Wakor.3: 10- 15.
3. Je, Ni nini baadhi ya masharti yaliyotolewa ambayo msingi huu uliwekwa? Ufu. 14:12, 12:17; Luka 9: 23-26.
4. Musa alionywa vipi kuhusu ujenzi wa hema ya Elohim? Kutoka 25: 8-9, 40; Waebr. 8: 5.
5. Ni nini itakuwa hali ya WaMasihi ikiwa alama za kale zitaharibiwa? Zab.11: 3, 82: 5.
6. WaMasihi wanashauriwa washindanie nini kwa bidii? Yuda 3.
7. Ni nini imetabiriwa kuhusu WaMasihi wengine ambao watatoka katika imani ya kweli? 1Tim.4: 1-3.
8. Waalimu hao wa uongo wanafananishwa na nini? Je, mtu anafaa kuendelea kushirikiana nao? 1 Tim. 6: 3-5; 2 Yohana 9-11.
9. Mtu anawezaje kutambua MMasihi wa uongo au mpinga Masihi? Luka 9: 49-50; Yohana 7:17; 1 Yohana 4: 1-3.
10. Katika siku za WaMasihi waliotangulia, watu fulani walijitahidije kuharibu alama za kale?Matendo.15: 1,5.
11. Wakati wazee wa hekima wa kanisa walichunguza ukweli juu ya jambo hilo, walifanya nini? Aya 2, 4, 6.
12. Katika mkutano wa dharura uliofanyika, ni azimio gani waliafikia? Aya 23-29.
13. Je ni shauri gani Paulo alitoa kwa watu waliosalia ambao wanashindana kwa bidii kwa imani ya zamani iliyotolewa kwa watakatifu? 1 Wakor.1:10.
14. Kwa nini Tito aliachwa Krete? Tito 1: 5.
15. Je, ni nini hatima ya wale watakaocha kwa makusudi mafundisho ya Injili? Wagal.1: 6-9; Warumi.16: 17-18; 2 Wathes.3: 6.
**********************
(Shevat 13, 5779)
NEEMA – ZAWADI KUU YA ELOHIM
Somo Kuu: Warumi 5: 1-21.
Fungu La Kukariri: Waroma 5:21.
1. Je, Ni tendo gani la kwanza limenakiliwa la neema kwa ajili ya mtu aliyeanguka? Mwanzo 3:21.
Fahamu: Uovu wa dhambi na matokeo yake; kifo kwa pande isiyo na hatia, imeelezewa katika aya hii fupi. Damu isiyo na hatia ilimwagika hili mtu aweze kupata mavazi ya mwili. Hivyo basi aina ya kwanza iliundwa katika Agano la Kale. Ililenga damu iliyomwagika ambayo inaweza kumsitiri mtu wa kiroho kama jinsi mahitaji yao ya kwanza yalitimizwa.
2. Jinsi gani tutajua ya kwamba Abili alipewa maagizo kuhusu mpango wa wokovu? Mwanzo 4: 4.
3. Uhusiano kati ya dhambi na neema ni nini? Rum 5: 17-20.
Fahamu: Kwa hakika kama jinsi dhambi na mauti zilikuja kupitia kuanguka kwa mwanadamu, zaidi ya hayo tunahakikishiwa kwamba itapita kwa sababu ya kifo na ufufuo wa Yahshua Mwana wa Elohim.
4. Hata katika nyakati za zamani, ni njia gani mbili zilikuwa wazi kwa mwanadamu? Kumb. 30:19;
Yer. 21: 8.
5. Je, Yahshua alielezeaje hilo jambo kwa Wayahudi? Yohana 5:40.
6. Ni ujumbe gani wa neema tunapaswa kuwa tunahubiri leo? Ufu. 22:17.
Fahamu: Tangia zamani Elohim amekuwa akifikisha neema yake kwa jamii ya wanadamu. Kwa nyakati zote akitekeleza neema yake kwa wanadamu. Tangia zamani wao walikataa rehema na upendo Wake hadi mwisho walimsulubisha Mwana wake mwenyewe. Tunapokaribia kurudi kwa mara ya pili, ndivyo dhabihu aliyoitoa itakataliwa zaidi. Hata hivyo kwa wale wanaomjua, Yeye bado ni yule Yule kama alipokuwa hapa duniani.
7. Je, Neema ya Elohim imefunuliwa kwa watu wangapi? Tito 2: 11-15.
8. Ni nini kinachoonyesha upendo usioweza kupimika ambao Masihi anao kwetu sisi? 2 Wakor. 8: 9.
9. Je, Jinsi gani neema imefunuliwa zaidi kwetu sisi? Mstari wa 12.
10. Je, Ni nini Paulo kwa njia ya unyenyekevu alikiri? 1 Wakor.15:10.
11. Alionyeshaje neema kwa siku za kale, za sasa, na za baadaye? 2 Wakor.1:10.
12. Katika kumkubali Masihi ni nini kinachowezekana kujua? Matendo 13:38, 39.
**********************
(Shevat 20, 5779)
NGUVU ZA ELOHIM ZA KUOKOA
Somo Kuu: Isaya 54: 4-17.
Fungu La Kukariri: Zaburi 103: 17.
1. Wakati miguu ya makuhani iligusa maji, ni nini kilichotokea kwa mto Yordani? Yoshua 3:15,16.
2. Ni wapi ambapo makuhani walipokuwa wakati wana wa Israeli walivuka mto wa Yordani?Mstari wa 17.
3. Je, Ni nini wanaume kumi na wawili, mmoja kwa kila kabila, waliamriwa kufanya? Yoshua 4: 5.
4. Je, Mawe yalikuwa yawakilishe nini, na wana wa Israeli waliamriwa kufanya nayo nini? Mstari wa 6-8.
5. Yoshua hatimaye aliweka mawe wapi? Mstari wa 9.
6. Je, wana wa Israeli walivukaje Yordani? Mst 10.
7. Ni lini na ni jinsi gani sanduku la Elohim, na makuhani, walivuka Yordani? Mstari wa 11.
8. Yoshua alisema nini ili watu wote wa dunia waweze kujua? Mst wa 24.
9. Je, Jinsi gani wana watatu wa Kiebrania waliokolewa katika tanuru ya moto? Danieli 3: 24-27.
10. Jinsi gani vinywa vya simba vilifungwa, ili wasiweze kumwangamiza mtumishi mwaminifu
wa Elohim, Daniel? Danieli 6:16, 19-23.
11. Ni kwa njia gani ya miujiza Paulo na Sila waliokolewa kutoka korokoroni? Matendo 16:25, 26.
Fahamu: Baba yetu wa Mbinguni ni wa ajabu, mwenye upendo, mwenye nguvu yote, tuna
fursa ya kumtumikia na kumtegemea katika maisha yetu yote! Hakubali mtu yeyote apotee,
lakini watu wote wanapaswa kuja kwake na kuokolewa. Hebu tujitahidi kujua na kufanya
mapenzi Yake na kuwasaidia wengine kuja katika nuru ya injili ya Masihi na utimilifu wake,
ili waokolewe.
***********************
(Shevat 27, 5779)
KUZAMISHWA (NDANI YA MAJI), NJIA YA ELOHIM YA UBATIZAJI
Somo Kuu: Mathayo 3.
Fungu La Kukariri: Wakolosai 2:12
1. Ubatizo wa Yahshua, jinsi gani ulifanywa na ulifanywa na nani? Mathayo 3: 13-16.
2. Mtume Paulo anasema nini kuhusu aina ya ubatizo katika siku alizoishi? Wakolosai 2:12.
3. Baada ya Pauli na Sila kufunguliwa kwa miujiza kutoka gerezani, ni mtu gani muhimu na familia waliamini na kubatizwa? Matendo 16: 29-33.
4. Tunapaswa kuenendaje baada ya kubatizwa, au kuzikwa pamoja Naye katika ubatizo? Warumi 6: 4.
5. Tutamvaa aje Masihi? Wagalatia 3:27.
6. Je, Sisi ni kwa kuzamishwa katika maji tumebatizwa katika kifo cha Masihi? Warumi 6:
3-4.
7. Kwa nani, na kwa namna gani, towashi aliyeamini alibatizwa? Matendo 8:38.
8. Ni aina ngapi za ubatizo zilizopo? Waefeso 4: 5.
9. Je, kulikuwa na watu wengi walioamini na kubatizwa baada ya kusikia mahubiri ya Petro
siku ya Pentekoste? Matendo 2:41.
10. Je, kulikuwa na wengine ambao waliamini na kubatizwa baada ya kusikia mahubiri ya Filipo juu ya ufalme wa Elohim na Yahshua Masihi? Matendo 8:12.
11. Kwa nini Yohana alibatiza huko Aenoni? Yohana 3:23.
Fahamu. Aya zilizo hapo juu zinathibitisha ukweli kwamba kuzamishwa ni njia sahihi ya ubatizo. Ikiwa kunyunyizia mtu maji hutosha, kwa nini Yohana alitaka maji mengi ya kubatiza? Kunyunyizia mtu maji ni makosa, na ni hali ya kusikitisha sana ambayo wengi wamewadanganywa na mafundisho hayo na bado wanataka kuyashikilia. Hebu tuombe ili waweze kuona mwanga wa kweli na kukubali nuru ya kweli na kukubali mpango wa Elohim wa wokovu kwa ukamilifu wake.
*******************
(Adar I 4, 5779)
NGUVU ZA ELOHIM KUPITIA ROHO MTAKATIFU
Somo Kuu: Wafilipi 2: 1-28.
Fungu La Kukariri: Wafilipi 2:15.
Fahamu.- Sura hii ambayo ni nzuri inatufundisha jinsi ya kushirikiana na wengine katika umoja wa kweli na furaha. Tafakari maneno haya: “Ikiwa kuna faraja yoyote katika Masihi, ikiwa faraja ya upendo, ikiwa ushirika wa Roho”, nk.
1. Je, Ni mambo gani manne ambayo ni muhimu ili kufikia umoja huu kama ulivyotolewa kwa Wafilipi. 2:2?
2. Badala ya kufanya kazi kupitia ugomvi na utukufu usiofaa, tunapaswa kufanya kazi zetu aje?Mst wa 3.
Fahamu. Maneno haya ni mazuri sana, “kwa hali ya unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.” Ikiwa tutafuata ushauri huu ambao ni bora, hakuwezi kuwa na ugomvi. Unawezaje (ugomvi) kuwepo?
3. Je, Ni ufanisi gani mzuri utatokea kutokana na mazoezi haya? Mst wa 4, 5.
4. Yahshua alijitukuza Mwenyewe kwa njia yoyote? Mstari wa 8.
5. Je, Ni nini kilichofuatia unyenyekevu Wake mkubwa? Mstari 9-11.
6. Ikiwa tunaweza kuwa na hatia katika uhusiano wetu sisi wenyewe, ni nini kitakachotokea katika hali zetu? Mstari wa 14, 15.
7. Ni hali gani nzuri iliyokuwapo kati ya ndugu katika siku za Paulo? Mstari wa 18-20.
8. Je, ni mashauri gani sawa yanayopatikana katika Wakolosai 3: 11-17?
9. Wakati Masihi anakaa ndani yetu katika Roho Mtakatifu, ni nini itakuwa matokeo siku zote? Yohana 15:4, 5.
10. Ikiwa hatutajitolea kushinda nafsi za watu kwa ajili ya Ufalme wa Elohim, matokeo yatakuwa yapi? Mstari wa 6.
11. Je, kushinda nafsi za watu itaongeza uwezo wetu tukiwa na Elohim kwa sala iliyojibiwa? Mstari wa 7, 8, 16.
*****************
(Adar I 11, 5779)
UWAKILI WAAMINIFU KATIKA MAFUNDISHO
Somo Kuu: Tito 1: 1-15.
Fungu La Kukariri: Tito 2: 1.
1. Je, Mtume Yuda alisema ni nini tunapaswa kushindania kwa bidii? Yuda 3.
2. Je, Ni aina gani mbili za mafundisho zilizoko hapa duniani? Mat. 7:28, 29;1 Tim.4: 1.
Fahamu. Katika maandiko haya mawili kumetajwa mafundisho ya Masihi, na mafundisho ya mashetani.
3. Je, Fundisho la Masihi ni gani kulingana na 1 Tim 6: 3-5?
4. Je, Yahshua alisema nini kuhusu mafundisho Yake? Yohana 7:16.
5. Kwa nini Alisema hivyo? Yohana 6:38; 5:30.
6. Ni kwa jinsi gani na ni kwa kupitia njia gani tutaweza kujua mafundisho ya kweli? 2Tim.3:16, 17.
7. Ni kwa njia gani Roho Mtakatifu anafanya kazi ya kufunua ukweli mzuri wa kuokoa? 2Pet.1:20, 21; Waebr.10:25; Ufu. 2: 7.
8. Je, kutii mafundisho mema kutatusaidia? Warumi 6:17, 18.
9. Kama watoto wa Elohim na walimu,
tumeamrishwa kufundisha nini? Tito 2: 1.
10. Je, mafundisho mazuri yanafaa kuhukumu kila
aina ya dhambi? Je! Dhambi ni nini? 1 Tim.1: 9-
10.
11. Kwa mafundisho mazuri tutaweza kufanya nini Tito 1: 9.
12. Ikiwa tutafuata mafundisho ya Biblia ya kweli,
yatafanya (mafundisho) nini? 1 Tim 4:16.
13. Je! Masihi Yahshua ni nini alituamuru kutoacha
bila kufanya? Mat. 23:23.
14. Ni kwa nini watu walishangaa kwa mafundisho
ya Masihi? Mat. 7:28, 29.
Maelezo.- Masihi alinena kwa mamlaka kwa sababu alifundisha Neno kwa usafi wake, na
hakuna mpinzani aliyetegemea mafundisho ya uwongo aliyefuzu kupinga mafundisho yake; hivyo ndivyo ilivyo kwa kila mtu hivi leo ambaye atafuata Neno lisilochafuliwa kama mwongozo
wake.
15. Jinsi gani Paulo alisema kuhusu watu kuyachukulia mafundisho mazuri wakati utakaokuja? 1 Tim.4: 1-4.
**********************
(Adar I 18, 5779)
UPENDO KATI YA MMOJA NA MWINGINE
Somo Kuu: Yohana 14: 15-31.
Fungu La Kukariri: Yohana 14:21.
1. Je, Ni nini moja ya sifa za Elohim? 1 Yohana 4: 8, 16.
2.Jinsi gani Elohim alidhihirisha upendo wake kwa ulimwengu? Yohana 3:16; Warumi 5: 8; Waefeso 2: 4,5.
3. Ni nini kinachohitajika kwa kila mtu anayekubali Masihi kama Mwokozi wake? Yohana 13:34; 15: 9, 10, 12.
4. Je, Dunia itawezaje kujua kwamba sisi ni wafuasi wa Masihi Yahshua? Yohana 13:35.
5. Ni kwa njia gani tutaupata upendo huu? Warumi 5: 5.
6. Je, Ni jambo gani pekee yake tumeshauriwa kuwa na deni kwa mtu yoyote? Warumi 13: 8 (sehemu ya kwanza).
7. Ni nini tunafanya wakati tunapopendana? Mstari wa 8 (sehemu ya mwisho).
8. Je, Bwana wetu alisisitizaje ukweli huu? Mathayo 22: 34-40.
9. Tunawezaje kuthibitisha upendo wetu kwa kila mmoja? Wagalatia 5: 14, 15.
Fahamu: Katika upendo wetu kwa Elohim, na mwanadamu mwenzetu, ndiyo utimilifu wa sheria zote na manabii. Ikiwa tunamdhuru ndugu yetu kwa njia ya kueneza uvumi ni dhahiri kwamba upendo ambao Elohim aliweka ndani ya mioyo yetu umepungua kwa kiasi fulani, kwa maana upendo haufanyi vibaya kwa jirani yake.
10. Je, Yahshua alisisitizaje upendo wake mkuu kwetu? Yohana 15:13.
11. Bwana ametuamuru aje sisi kupendana? Aya 12.
12. Je, Upendo huu utasababisha sisi kuvaa nini? Wakolosai 3:12.
*********************
(Adar I 25, 5779)
UNYENYEKEVU DHIDI YA KIBURI
Somo Kuu: Danieli 4: 19-37.
Fungu La Kukariri: Mithali 16:19.
1. Je, Ni mambo gani mengine ambayo Sulemani alisema kuwa huja kutokana na kiburi? Mithali 11: 2; 13:10
2. Je, Kiburi na unyenyekevu zina tofauti gani? Mithali 29:23.
3. Daudi alisema nini juu ya kiburi? Zaburi 10:2; 12:3, 4; 73:3-6.
4. Je, Ni nini kilichotokea kwa Farao kwa sababu ya kiburi chake? Kutoka 5:2; 14:8, 28.
5. Je, kiburi kilimfanya mfalme Uzia kufanya nini, na matokeo yake ya mwisho yalikuwa nini? 2 Mambo ya Nyakati 26:16, 19, 21.
6. Ni kwa nini ghadhabu ilinenwa juu ya Israeli wakati wa utawala wa Hezekia? 2 Mambo ya Nyakati 32: 24-26.
7. Je, Yahshua alifundisha somo gani la unyenyekevu? Luka 14: 7-11.
8. Paulo alitoa ushauri gani wa unyenyekevu? Warumi 12: 3; 11: 18-21.
9. Ni nani ambaye Nabii Isaya alisema kuwa Mtakatifu atakaa ndani yake? Isaya 57:15.
10. Ni kitu gani muhimu wenye dhambi wanafaa kufanya ili waweze kuwa watoto wa Elohim?
Mathayo 18: 3,4; Yakobo 4:10.
11. Ni jambo gani la unyenyekevu ambalo Yahshua alionyesha muda mfupi kabla ya kusulubiwa
kwake? Yohana 13: 3-5.
12. Ni adhabu gani kali iliyotolewa kwa Mfalme Herode kwa sababu ya kukosa kumtukuza Elohim? Matendo 12: 21-23.
13. Je, Ni ushauri gani Yahshua anawapa wenye kiburi? Ufunuo 3: 17, 18.
Fahamu: Huwa inasemekana: “Ulimi hutuingiza katika shida na kiburi huendelea kutuweka
katika shida.” Hilo lisiwe kweli kwa wana wa Elohim. Hebu tukumbuke kwa nyakati zote
maneno ya Sulemani “Hekima hukaa na wanyenyekevu.” Mithali 11: 2.
***********************
Somo la Machi 9, 2019 (Adar II 2, 5779)
KUYAWEKA MAZUNGUMZO YETU KUWA MEMA
Somo Kuu: Yakobo Sura ya 3
Fungu La Kukariri: Zaburi 50:23.
1. Jinsi gani maneno yetu ni muhimu? Mathayo 12:37.
2. Maneno yetu huja kutoka wapi? Mathayo 12:34, 35.
3. Je, Sala ya Mfalme Daudi ilikuwa nini kuhusu mawazo ya moyo wake na maneno ya kinywa chake? Zaburi 19:14.
4. Amri ya tisa inakataza nini? Kutoka 20:16.
5. Ni kwa njia gani Bwana Elohim aliwaonya wana wa Israeli kuhusu ulimi? Mambo ya Walawi 19:16.
6. Je, Maneno ya mchongezi hufananishwa na nini? Mithali 26: 21-22; 17: 9.
7. Je, ni athari gani itakayotokea kwa kukosa kueneza uvumi kwa watu wanao ugomvi? Mithali 26:20.
8. Sulemani, mtu mwenye hekima, alizungumzia nini maneno yaliyofaa (kwa hekima) yakiongewa? Mithali 25:11.
9. Je, ni tofauti gani kubwa kati ya mazungumzo kutoka midomo ambayo inayodhibitiwa na Bwana na ile ambayo haidhibitiwi? Isaya 57: 19-21.
10. Anajulikana aje yule awezaye kudhibiti ulimi wake? Yakobo 3: 2.
11. Kwa nini WaMasihi wanapaswa kuwa makini sana juu ya mazungumzo yao? Mathayo 12:36, 37.
12. Je, Bwana Elohim wetu anajua yote kuhusu maneno yetu? Zaburi 139: 4.
Fahamu. Kitu kimoja ambacho kinaonekana kuwa rahisi na asili kwa watu wengi kufanya ni
kuzungumza kwa upumbavu. Kuna mambo mengi sana ya kusema ambayo itafurahisha watu
na kuwafanya wacheke. Hii ni moja ya furaha kubwa ya watu wa kidunia, lakini WaMasihi
wana furaha zaidi na zaidi kuliko hii, na haifai kwao kuwa na mazoea ya kuongea maneno
kama hayo ya kipumbavu.
13. Ni pamoja na nini dhambi nyingine za msingi, mazungumzo ya kipumbavu imelinganishwa?
Waefeso 5: 3, 4.
******************************
Somo la Machi 16, 2019 (Adar II 9, 5779)
TINI NZURI NA TINI MBAYA
Somo Kuu: Yeremia 24.
Fungu La Kukariri: Yeremia 24: 7.
1. Tini nzuri ni aina gani? Yer. 24: 5-6.
2. Je, tini nzuri zilifaa kupokelewa bora zaidi kuliko zile zilizo mbaya? Mstari wa 7.
3. Je, Ni sehemu gani ya Yuda iliwakilishwa na tini mbaya? Mstari wa 8.
4. Je, jinsi gani tini mbaya zilifaa kuadhibiwa, na je, kuna yoyote ingebaki? Mstari wa 9 na 10.
Fahamu: Kutoka kwa maandiko yaliyotangulia ni wazi kwamba kulikuwa na makundi mawili tofauti ya Wayahudi katika uhamisho, na ahadi zilikuwa tofauti kwa kila kundi. Yeye bado anaweza kutenganisha nzuri kutoka kwa mbaya, kama ilivyofanyika wakati wa kale, Yeye anafanya hivyo leo.
5. Ni kundi gani la Wayahudi lilipaswa kuchaguliwa ili kujenga miji iliyokuwa ukiwa na kufanya kazi ambayo tunaona inaendelea hapa sasa? Yeremia 24: 1-7.
6. Ni mapigo mangapi yalifanyika katika kuharibu ufalme wa Yuda? Ezekieli 21: 25-27. Linganisha
2 Mambo ya Nyakati 36: 15-19.
Fahamu: Huwa inasemekana juu ya maadui wa mataifa kwa Israeli: “Kama ulivyotenda ndivyo utakavyotendewa.” - Obadia 1:15; Yoeli anasema: “Nitakurudishia malipo yenu juu ya kichwa chako mwenyewe.” - Yoeli 3: 7.
7. Katika uharibifu huu wa ufalme wa Israeli miaka 2,500 iliyopita, wale waliolinganishwa na tini
mbaya walichukuliwa kwanza au mwisho? Linganisha Yer. 24: 8 na 2 Mambo ya Nyakati
36: 11, 12, 16.
Fahamu: Zedekia na wakuu wake walikuwa ni tini mbaya, na waliachwa, wakati tini nzuri ziliondolewa, kama itakapokuwa mwishoni, mema yatachukuliwa kwanza.
8. Ni lini tini nzuri, ikiwa ni pamoja na Danieli na wenzake, na wengine wengi walichukuliwa?Danieli 1: 1-6.
Fahamu: Waliondolewa na Mfalme Yehoyakimu na hawakuachwa Yerusalemu wakati uharibifu mbaya ulikuja ambapo wanaume, wanawake na watoto walitolewa kwa upanga.
9. Ni nini hasa kinachosemwa kuhusu tabia ya Chakula cha Danieli? Danieli 1: 7-8.
10. Kabla ya uharibifu mkubwa wa waovu mwishoni mwa kipindi cha mataifa, je,
watakatifu watakusanywa kwanza? Ufunuo 14:18.
11. Baada ya mkusanyiko wa matunda umekusanyika basi ni nini kitachotokea kwa
waovu ikilinganishwa na mzabibu wa dunia? Mstari wa 19 na 20.
12. Ni wapi tunaambiwa kuwa watakatifu watakuwa, ambao wana ushindi juu ya mnyama
na sanamu yake, wakati mapigo yatamwagwa? Ufunuo 15: 1-6.
Fahamu: Angalia hasa mstari wa 5 inasema: “Baada ya hayo”, yaani, baada ya watakatifu walipoonekana mahali hapa ambapo ilionekana kama bahari ya kioo kwa nabii, aliwaona malaika wakitoka na mapigo saba ya mwisho - Mstari wa 6. Baini pia vita ya Armageddon vinakuja katika wakati wa pigo la sita. – Ufunuo 16: 12-15. Kwa hivyo wenye haki wanaonekana wamekusanyika mahali Fulani katika ukombozi kutoka kwa maafa haya. Hakuna kitu ambacho kimesemwa mahali hapa ni wapi, wala haimaanishi kuwa walichukuliwa juu kama tunavyosikia mara nyingi ikinukuliwa.
******************************
Somo la Machi 23, 2019 (Adar II 16, 5779)
KUCHUKULIWA MIMBA NA KUZALIWA KWA YAHSHUA
Somo Kuu: Mathayo 1: 16-25.
Fungu La Kukariri Mathayo 1:18.
1. Je, Malaika alimpa Mariamu ujumbe upi? Luka 1: 28-31.
2. Je, Mariamu alishangaa na kile ambacho malaika alimwambia? Luka 1:34; Matayo.1:18.
Fahamu. Maandiko Matakatifu yanatuambia kwamba Mariamu alikuwa bikira aliye safi sana kwamba hakujua mtu. Alikubali kuolewa na Yusufu, lakini kabla ya kumjua kama mkewe, alipata mtoto na njia ya Roho Mtakatifu. Matayo.1: 18-20; Luka 1:35.
3. Je, Ni uhusiano gani ulikuwa kati ya Yusufu na Maria kabla ya kuzaliwa kwa Yahshua? Ni nini ambacho kilikuwa chanzo cha mimba ya Masihi? Matayo.1:18; Luka 1:35.
4. Je, Isaya alitabiri nini juu ya tukio hili la ajabu? Isa.7:14; linganisha na Matayo.1:23; Luka 1:31.
5. Je, Yusufu alitaka kufanya nini? Matayo.1:19.
6. Ni nini malaika wa Bwana alimwambia Yusufu katika ndoto? Matayo.1: 18-25.
7. Wakati Yusufu na Maria walipofika Bethlehemu walipokelewa aje? Luka 2: 4-8.
8. Ni jina gani alilopewa mtoto na malaika hata kabla hajazaliwa? Matayo.1:25.
9. Je, umuhimu wa jina hili umesisitizwa aje? Matendo 4: 10-12: Wafilipi. 2: 9-11.
10. Je, Paulo alisema nini kuhusu utimilifu wa hili? 1 Tim.3:16.
Fahamu. Unabii huu na utimilifu wake umekuwa lengo la wasioamini na watu wa
kisasa kwa karne nyingi. Hapa nguvu ya Elohim ilidhihirishwa na mimba ya kimiujiza na kuzaliwa
kwa Mwana wake mpendwa, Yahshua. Mara kwa mara, Yahshua aliwambia wasikilizaji wake kwamba alikuja kutoka juu na kwamba Elohim alikuwa Baba Wake.
11. Je, Ni nini kilichotokea wakati wachungaji walikuwa wakilinda kondoo zao? Luka 2: 8-14.
12. Walipata tukio gani na malaika? Je, Hii ilikuwa na athari gani? Luka 2: 9.
13. Je, Ni ishara gani waliyopewa kuhusu mtoto huyu? Luke 2:12.
14. Je, Ni eneo gani lenye utukufu ambalo wachungaji waliruhusiwa kushuhudia? Luka 2: 13-14.
15. Jinsi gani malaika walionyesha furaha yao kwa wakati huo, ni nini kilichofanyika? Luka 2:14.
16. Wachungaji wa kondoo waliitikiaje tangazo hili? Luka 2: 16-20. Je, hii inafaa kuwa mfano kwetu
sisi? Isaya 12.
******************************
Somo la Machi 30, 2019 (Adar II 23, 5779)
MAOMBI YA MASIHI ILI ATUKUZWE
Somo Kuu: Yohana 17.
Fungu La Kukariri: Yohana 17: 5.
1. Ni nini Yahshua Masihi alimwomba Baba wa Mbinguni? Yohana 17: 1.
2. Je, Ni nguvu gani imepewa Masihi na Baba? Yohana 17: 2.
3. Uzima wa milele ni nini? Mstari wa 3.
4. Ni kwa namna gani Masihi alimtukuza Baba? Mstari wa 4.
5. Masihi aliendeleaje kumwomba Baba? Mstari wa 5.
6. Je, Masihi alidhihirisha nini ambacho Baba yake alimpa kwa watu? Mstari wa 6.
7. Je, ni jambo gani lingine muhimu sana na la kuhitajika alilowaletea kutoka kwa Baba? Mstari wa 8 (sehemu ya kwanza).
8. Je, waliamini na kumpokea? Mstari wa 8 (sehemu ya mwisho).
9. Je, aliomba peke yake? Mstari wa 9.
10. Katika sala yake kwa Baba, kwa ajili yao, alimwomba afanye nini? Mstari wa 11.
11. Jinsi gani wafuasi wake walihifadhiwa wakati alipokuwa duniani? Mstari wa 12.
12. Je, Ulimwengu ulikuwa na mtazamo gani kwao? Mstari wa 14.
******************************
© 2012 Church of Elohim 7th Day ~ Powered by Kenesiyahmessenger ~ Powered by wix