
Bible Lessons
for
THE CHURCH OF ELOHIM
7th Day
————
1st Quarter
2020
—————
FOR
Tevet, Shevat, Adar, Nisan
(January, February, March.)
To be used with the Bible
—————
Workers are needed, for the harvest
is great, but laborers are few...
—————
Address all orders to P.O. Box 568,
Jerusalem — Israel
_____________
Lesson for January 4, 2020.
THE PROMISED SEED
Scripture Reading: Romans 11:1-25.
Memory Verse: Romans 11:27.
1. What proportion of Israel did the Lord say would be saved? Isaiah 10:21,22; Romans 9:27.
2. What is said of their spiritual standing? Romans 10:2
3. How long were they given to settle their acceptance with Elohim as a nation? Daniel 9:24.
4. From what year were the seventy weeks to be numbered? Daniel 9:25.
5. What would happen to the Messiah near the end of the seventy weeks? Daniel 9:26.
6. How long would the Abrahamic covenant be confirmed? What would happen in the midst of the last prophetic week? Daniel 9:27.
NOTE: This is 70 prophetic weeks, or 490 years. This rule of counting is found in Numbers 14:34, where the Lord gives a day for a year. Counting from the going forth of the year which was 457 B.C., 490 years would extend to 33 A.D. Sacrifices were to cease in the midst of the 70th week, and this was the date of the Crucifixion.
7. After this probationary time is ended, what would be evident in their experience according to prophecy? Romans 11:8-12,15.
8. As a result of their falling and breaking off, what has come to the Gentiles? Romans 11:17,19,20.
9. What promise is still held out to them? Romans 11:23,24.
10. How long will this blindness remain on them? Romans 11:25.
11. Whom did Paul say would be saved? Romans 11:26.
12. What will save them? Romans 11:17-20; Romans 9:32; Ephesians 2:8,9,16-19.
*******************************
Lesson for January 11, 2020.
THE HOUSE OF DAVID
Scripture reading: Psalms 89:1-37.
Memory verse: Revelation 22:16.
1. From what tribe of Israel was David? Matthew 1:3-6.
2. Who anointed him king over Israel? 1 Samuel 16:13; Psalms 89:20.
3. Because of his faithfulness, what did the Lord promise him? 2 Samuel 7:8, 12-16.
4. What is written in the Psalms about this covenant? Psalms 89:3,4,27,29.
5. If his descendants sin what will be the results? Psalm 89:30-32.
6. Will this cause the good Lord to break His covenant? Psalms 89:33-34.
7. How long will this covenant with David continue? Psalms 89:35-37.
8. Will he ever want a son to sit on his throne? Jer. 33:21
9. How sure is this covenant? Jer. 33:19-22.
NOTE. The Sun, Moon and stars are still in the firmament, so must David’s seed always be on the throne.
10.What descendants of David shall finally sit on his throne? Matthew 1:1; Isaiah 9:6, 7.
11.How long will His reign continue? Luke 1:31-33.
12.Into what reign will His kingdom finally blend? 1 Co. 15:24; Zec. 14:9.
*******************************
Lesson for January 18, 2020.
THE PRICE AND RESULT OF PRIDE
Scripture reading: Psa. 10.
Memory verse: Prov. 28:25.
1. How are the evils of the proud described in Elohim's Holy Word? Isa. 2:11-13.
2. What did pride bring to a city of Moab? Jer.49:13-16.
3. What is the source of all pride? 1 John 2:16.
4. What is listed first among the seven things which the Lord hates? Prov. 6:16, 17.
5. What will pride do to the person who is filled with it? Prov. 16:5.
6. What did pride bring to Nebuchadnezzar? Dan. 5:18-21.
7. Instead of endeavoring to lift ourselves to high stations in this life, what should we be doing? Rom. 12:16.
8. How does true, genuine honor come to the faithful of the Lord our Elohim 1 Pet. 5:1-4.
9. Even though man may be in a high place and state, does it excuse him for being proud? Psa. 39:5; 18:27.
10. Does a man’s greatness consist of the things he possesses? Luke 12:15.
11. What will happen to the exalted man who trusteth in himself? Luke 12:16-21.
Lesson for January 25, 2020.
THE REWARD OF ACCEPTING YAHSHUA
Scripture reading: Matt. 19:23-30.
Memory verse: Matt. 16:27.
1. What is the bounteous reward of forsaking all and following Yahshua Matt. 19:27-29.
2. What else is necessary in order to receive this reward? Matt. 10:37-39.
3. Does our labour for Him necessarily have to be of a great nature? Verse 42.
4. Are there limitations as to what we can do? 1 Cor. 3:6, 7.
5. Who then is our great Co-worker? Verses 8 and 9.
6. What warning has been given in connection with our work with Messiah Yahshua ? Verse 10.
7. Should one ever consider starting a work of his own? Verse 11.
8. What is the advantage of having one’s work grow into that which is to be permanent? Verses 13, 14.
9. What are some other admonitions given in this chapter as to the manner in which we are to labor for Him? Verses 18, 19, and 21.
10. What encouragement did the prophet Azariah give to King Asa at one time? 2 Chron. 15:1-7.
11. What was the happy result? Verses 8-15.
12. In what kind of work must we abound, and will it be in vain? 1 Cor. 15:58.
13. Is there a record in heaven of our work, and our prayers here on earth? Acts 10:1-4.
Lesson for February 1, 2020.
THE POWER OF THE SPIRIT IN THE LIFE
Scripture reading: Romans 8:1-14.
Memory verse: Romans 8:11.
1. In order to be free from condemnation, how must the people of Elohim walk? Rom. 8:1.
2. How can we judge rightly and know that we are walking in the spirit? Rom. 8:4.
3. What is the reward — both temporal and eternal to those who are spiritual-minded? Rom 8:6.
4. What is a sure index of a person’s life? Matt. 12:34, 37.
5. What should be the daily prayer of everyone seeking a home in the Kingdom of Elohim Psa. 19:14.
6. When the people of the Lord are spiritual-minded, what will their conversation be? Psa. 50:23.
7. Is it possible to please Elohim when we are in the natural ways of the flesh? Rom. 8:8.
8. What is it that is necessary to abide in each child of Elohim that he may not follow the flesh? Rom. 8:9.
9. If this spirit takes up its abode within us and remains, what work will finally be wrought? Rom. 8:11.
10. How can we acquire the indwelling of the Holy Spirit? Luke 11:11-13.
11. What important Messianic virtue does the Holy Spirit shed abroad in our hearts? Rom. 5:5.
12. In what way and by what power can we overcome the natural ways of the flesh? Rom. 8:13, 14.
13. When led by the Spirit, where will we be storing our treasures? Matt. 6:19-21.
*******************************
Lesson for February 8, 2020.
THE LIFE OF THE APOSTLES
Scripture Reading: Acts 2.
Memory Verse: Acts 2:42.
1. Whose example did the Apostle Peter say that the followers of the Lord should use? I Peter 2:21; I John 2:6; Ephesians 5:1.
2. In following the steps of Yahshua how zealous and enthusiastic were the apostles of Yahshua in response to the heavenly calling? Matthew 4:18-22; Mark 10:28.
3. After forsaking their private engagements (works) for the sake of the Gospel, how did some, who were servants and top officials of the government of their country react? Luke 5:27-32; Philippians 3:7,8; Luke 19:1-8.
4. Through what means were these devoted disciples of Yahshua earning their livelihood? I Corinthians 4:12; Acts 18:3.
5. Was there a unanimous and singleness of mind and heart in their midst? Acts 4:32; 2:46.
6. What was the apostle’s attitude towards the calamity and welfare of their fellow-brethren? Ephesians 1:15-19.
7. How did they suffer for the sake of Yahshua and the Gospel? Hebrews 11:36-38.
8. How generous were they? Acts 2:45; 4:32.
9. How did they behave themselves towards the souls which were won to the Lord through their preaching? 1 Thessalonians 2:2; 5:7-10.
10. What was their attitude towards persecution, afflictions and those who maltreated them? Acts 5:40, 41; 2 Corinthians 12:10.
11. How did Matthias get numbered with the eleven apostles? Was it by partiality, nomination, nepotism, voting or by casting of lot? Acts 1:23-26.
12.How did they regard the assembling together of the brethren? Acts 2:42-46.
*******************************
Lesson for February 15, 2020.
PETER - FISHER OF MEN
Scripture reading: John 21:3-17.
Memory verse: Matthew 4:19.
1. Matthew 4:18-20 tells of the calling of Simon Peter and his brother Andrew. With what intriguing promise did Yahshua call them? How did they respond?
2. Compare this account with John 1:35-42.
3. Discuss the occasion, the account of which Matthew 14:28 is a part. Does it reveal Peter’s character?
4. Perhaps the most glorious part of Peter’s association with Yahshua is recorded in Luke 9:28-36. How did he regard it? Why did they keep it a secret? Matthew 17:9.
5. What was the most bitter experience in his association with Yahshua Matthew 26:69-75.
What was the result of this experience in Peter’s life?
6. What was Christ’s charge to Peter? John 21:15-17.
7. Did Peter obey this command? Discuss Acts 2:14, 37-40; 5:12-16.
8. How does Peter’s admonition in 2 Peter 3:11-14 conform to his own life? Is it sound advice?
Lesson for February 22, 2020.
PAUL, THE GREAT EVANGELIST
Scripture Reading: Acts 9:10-20.
Memory Verse: 2 Timothy 4:7.
1. What do we know about Paul’s early life? Acts 22:3. Smith’s Bible Dictionary suggests that he was probably taken to Jerusalem as a boy for his education.
NOTE: Saul means “asked, “Desired”. Paul means “small” or “little”. These names are very appropriate to the life of the Apostle. He was desired of men, very prominent and highly trusted by the leaders. After his conversion, however, he was very humble.
2. Discuss the following points in the story of Paul’s conversion (Acts 9).
i. The mission to Damascus.
ii. Saul’s vision.
iii. Ananias’ part.
3. What did Paul do? Why did he leave Damascus? Acts 9:22-25.
4. How was he received at Jerusalem, and where did he go from there? Acts 9:26-30.
5. Discuss Acts 11:19-30; 12:24-25; 13:2,3.
6. Did they carry out their mission? Romans 15:25- 28; 1 Corinthians 16:1-3; 2 Corinthians 8:1-5; 9:1-12.
7. Discuss Acts 20:22,23; 21:10,11,33.
NOTE: From the day that Agabus’ prophecy was fulfilled in A.D. 58, Paul was a prisoner of the Roman Empire until the year 63, at which time he was permitted to dwell in his own house (Acts 28:30). He was again arrested in A.D. 65 and beheaded in A.D. 67or 68.
8. What have you to say about his conduct while he was under arrest.
*******************************
Lesson for February 29, 2020.
PAUL’S FINAL MESSAGE TO THE CHURCH
Scripture Reading: 2 Timothy 4:1-8.
Memory Verse: 1 Timothy 5:7.
1. Before whom did Paul give his final charge, and at what time did he say the living and the dead would be judged? 2 Timothy 4:1.
2. What did he admonish his people to preach, and what of the use of doctrine? 2 Timothy 4:2.
3. What prophecy did he give of the people’s attitude towards sound doctrine? 2 Timothy 4:3.
4. How did he say the people of the last days would generally consider truth, and to what would they be turned? 2 Timothy 4:4.
5. How did he instruct Timothy relative to affliction in connection with the work before him? 2 Timothy 4:5.
6. Was Paul reconciled to his fate and ready to lay down his life? 2 Timothy 4:6.
7. Was he thoroughly satisfied with the battle of his life he had so incessantly fought, and did he know he had won the victory? 2 Timothy 4:7.
NOTE: Every child of Elohim should be satisfied with his life. He should know day by day that he is fighting the good fight of faith.
8. What was now Paul’s great comfort and hope, and to what time did he look, expectant of receiving his reward? 2 Timothy 4:8 [last part].
9. Who was it that stood by Paul, giving him strength to fight the battle of life? 2 Timothy 4:17.
10.Was Paul the most concerned about deliverance from afflictions or from evil work? 2 Timothy 4:18.
11. In Paul’s last admonition to Titus what did he say about denying ungodliness and lust? Titus 2:12.
Lesson for March 7, 2020.
THE TIME OF THE END AND DELIVERANCE
Scripture Reading: Psalms 91.
Memory Verse: Daniel 12:1.
1. Just before the dead are resurrected, what conditions will prevail on the earth? Daniel 12:1,2; Revelation 11:18.
2. What city will be made burdensome to all nations; against which they will direct their armies during the time of trouble? Zechariah 12:2,3; 14:1-3.
3. What is especially said about those who are wise in the knowledge of Elohim during the time of the end? Daniel 12:3, 4, 10.
4. What is further said of Elohim's watchmen? Isaiah 52:8, 9.
5. What is said about the chariots (modern means of travel), when the message of Elohim's preparation is going forth in these last days? Nahum 2:3, 4.
6. What is prophesied about the troubled condition of the hearts of men, and distress in the nations of the world, just before the coming of the Lord? Luke 21:24-27.
7. When the time of trouble is threatening throughout the world, what will the nations be doing to try to prevent disaster? Isaiah 8:9,10.
8. What does the Lord say for His people not to do? Verse 12.
9. Who are we to look upon for help? Verse 13; Zephaniah 2:3.
10.What particular message will Elohim's people be deeply concerned about? Isaiah 8:16.
11.By what great standard are people of earth to be judged by? Verse 20; Revelation 12:17; 14:12.
12.What will happen to the unprofitable servant at that time? Matthew 25:30; Luke 12:46.
13. What will be the condition throughout the earth as Gentile times end? Luke 21:26, 27, 34, 35.
14. In order for deliverance, what are we commanded to do? Luke 21:36.
******************************
Lesson for March 14, 2020.
THE RESURRECTIONS
Scripture reading: 1 Cor. 15:1-58.
Memory Verse: 1 Cor. 15:22
1. Will everybody be resurrected? John 5:28, 29.
2. When will the righteous be resurrected unto life eternal? 1 Cor. 15:22-23; Rev. 20:4-6; 1 Thess. 4:16.
3. What will happen to the saints who will be alive at the appearing of Yahshua 1 Thess. 4:17; 1 Cor. 15:51-53.
4. Where will the resurrected saints dwell, and what will be their work during the millennium? Rev. 5:10; Dan. 7:27.
NOTE. What a wonderful blessing awaits all the faithful in Messiah Yahshua! All who have died in the lord will be made alive at the appearing of Yahshua , while the living saints will be changed in a moment, in the twinkling of an eye, and they will live and reign with Messiah for a thousand years. During this time Yahshua will be reigning upon the throne of David.
5. Where will the wicked dead be during this millennial reign of the Lord Yahshua Rev. 20: 5,6.
Lesson for March 21, 2020.
WHICH DAY IS THE SABBATH?
Scripture reading: Hebrews 4:1-16.
Memory verse: Jer. 17:21-22.
1. Can we tell what day is the Sabbath? Matt. 28:1.
2. Did Moses know what day was the Sabbath before it was given on Mt. Sinai? Exod. 16:23- 25.
3. How long was the Sabbath day to be kept? Exod 31:16, 17.
NOTE: Perpetual means unending; no end to it.
4. Will the Sabbath day be kept in the Millenium reign of the Saviour? Isa. 66:23.
5. What is the sign to the people to prove they are sanctified (set apart)? Ezek. 20:12, 20; Exod. 31:13, 14.
6. What did the Saviour say in regard to the Sabbath? Was it just for the Jews, or for all men? Mark 2:27.
7. Did the Saviour have respect for the Sabbath day? Matt. 24:20; Luke 4:16-18.
NOTE: Jerusalem was destroyed in the year 70A.D., and He did not want their flight to be on that day.
8. Did the holy women keep the Sabbath day after the Saviour was put in the grave? Luke 23:55- 56.
9. Did Paul keep the Sabbath day, and did he say it still remained? Acts 13:42-44, 16:13-15, 18:1-4; Hebrews 4:9.
10.Were people put to death for working on the Sabbath? Numbers 15:32-36.
NOTE: The Sabbath is still sacred and binding today just as it always was, and it is an act of disobedience to desecrate it. Six days are given to us for our work, but the Sabbath belongs to the Lord, and is not our property. We have no right to covet it, or to steal it, and use it for our own labour and business.
*******************************
Lesson for March 28, 2020.
THE SOURCE AND NEED OF BIBLE PROPHECY
Scripture reading: 2 Peter 1:1-21.
Memory verse: 2 Peter 1:21.
1. How is all Scripture given? 2 Timothy 3:16.
2. For what purpose are they given? 2 Timothy 3:17.
3. Are these prophecies for us today? And what will they do? Deuteronomy 29:29.
4. What is the last book in the Bible called? Revelation 1:1.
5. What did the Lord Elohim promise those who read these prophecies? Revelation 1:3.
6. How are the Old Testament prophecies given? 2 Peter 1:21.
7. What is said of the interpretation of these prophecies? 2 Peter 1:20.
8. Did the Spirit of Messiah have anything to do with the prophets? 1 Peter 1:11.
9. How was the coming of Messiah revealed to Peter?1 Peter 1:11, 12.
10. What are these prophecies to us in our day? 2 Peter 1:19; 1 Corinthians 10:11; Romans 15:4.
11. Will the true elect person, called of the Heavenly Father for eternal life, be fruitful or unfruitful in the work of the Lord at this time? 2 Peter 1:8.
*******************************
Bible Lessons
for
THE CHURCH OF ELOHIM
7th Day
Kiswahili
1st Quarter
2020
—————
FOR
Tevet, Shevat, Adar, Nisan
(January, February, March)
To be used with the Bible
—————
Workers are needed, for the harvest
is great, but laborers are few...
—————
Address all orders to P.O. Box 568,
Jerusalem — Israel
_____________
Januari 4, 2020 (Tevet 7, 5780)
MBEGU ILIYOAHIDIWA
Somo Kuu: Warumi 11: 1-25.
Fungu La Kukariri: Warumi 11:27.
1. Ni asilimia ngapi ya Israeli ambayo Bwana alisema ingeokolewa? Isaya 10: 21, 22; Warumi
9:27.
2. Je! Ni nini imesemekana kuhusu msimamo wao wa kiroho? Warumi 10: 2
3. Walipewa muda gani ili kukubaliwa na Elohim kama taifa? Danieli 9:24.
4. Je! majuma sabini yalihesabiwa kutoka mwaka gani? Danieli 9:25.
5. Je! Nini ingetokea kwa Masihi majuma haya sabini yakikaribia kuisha? Danieli 9:26.
6. Agano la Abrahamu litathibitishwa kwa muda gani? Nini ingetokea katikati ya juma la mwisho
la unabii? Danieli 9:27.
Maelezo: Haya ni majuma 70 ya unabii, au miaka 490. Sheria hii ya kuhesabu inapatikana
katika Hesabu 14:34, ambapo Bwana huhesabu siku moja kama mwaka mmoja. Ukihesabu
kutoka mwanzo wa mwaka ambao ulikuwa 457 B.C, miaka 490 ingefikia hadi 33 A.D. Sadaka
zilikomeshwa katikati ya juma la 70, na hii ilikuwa tarehe ya kusulubishwa.
7. Baada ya wakati huu wa kumalizika, nini itadhihirika katika hali yao kulingana na unabii?
Warumi 11: 8-12,15.
8. Kama matokeo ya kuanguka kwao na kukatwa, ni nini imekuja kwa Mataifa? Warumi 11:
17,19,20.
9. Ni ahadi gani ambayo bado wamewekewa? Warumi 11: 23,24.
10. Huu upofu utabaki kwao hadi lini? Warumi 11:25.
11. Paulo alisema ni nani ataokolewa? Warumi 11:26.
12. Ni nini kitakachowaokoa? Warumi 11: 17-20; Warumi 9:32; Waefeso 2: 8,9,16-19.
******************************
Somo la Januari 11, 2020 (Tevet 14, 5780)
NYUMBA YA DAUDI
Somo Kuu: Zaburi 89: 1-37.
Fungu La Kukariri: Ufunuo 22:16.
1. Daudi alikuwa wa kabila gani la Israeli? Mathayo 1: 3-6.
2. Ni nani aliyemtia mafuta kuwa mfalme wa Israeli? 1 Samweli 16:13; Zaburi 89:20.
3. Kwa sababu ya uaminifu wake, Bwana alimwahidi nini? 2 Samweli 7: 8, 12-16.
4. Je! Imeandikwa nini katika Zaburi kuhusu agano hili? Zaburi 89: 3,4,27,29.
5. Ikiwa kizazi chake kitatenda dhambi ni nini itakuwa matokeo? Zaburi 89: 30-32.
6. Je! Hii itamfanya Bwana mwema avunje agano lake? Zaburi 89: 33-34.
7. Agano hili kwa Daudi litaendelea hadi lini? Zaburi 89: 35-37.
8. Je! Atataka mwana wa kiume aketi katika kiti chake cha enzi? Yer. 33:21
9. Je! Agano hili lina uhakika gani? Yer. 33: 19-22.
Maelezo. Jua, Mwezi na nyota bado ziko kwenye anga, kwa hivyo lazima uzao wa Daudi uwe
kwenye kiti cha enzi kila wakati.
10. Je! Ni wazao gani wa Daudi ambao watakaa kwenye kiti chake cha enzi? Mathayo 1: 1; Isaya 9:
6, 7.
11. Utawala wake utaendelea hadi lini? Luka 1: 31-33.
12. Je! Ufalme wake hatimaye utajumuishwa katika ufalme gani? 1Wakorintho 15:24; Zek. 14: 9.
******************************
Somo la Januari 18, 2020 (Tevet 21, 5780)
GHARAMA NA MATOKEO YA KIBURI
Somo Kuu: Zab. 10.
Fungu La Kukariri: Met. 28:25.
1. Je! Uovu wa wenye kiburi umelezewaje katika Neno Takatifu la Elohim? Isa. 2: 11-13.
2. Kiburi kilileta nini kwa mji wa Moabu? Yer. 49: 13-16.
3. Je! Ni nini chanzo cha majivuno yote? 1 Yohana 2:16.
4. Ni nini kilichoorodheshwa kwanza kati ya vitu saba ambavyo Bwana anachukia? Methali. 6:16,
17.
5. Kiburi kitafanya nini kwa mtu ambaye amejawa nacho? Methali. 16: 5.
6. Kiburi kilimletea nini Nebukadreza? Dani. 5: 18-21.
7. Badala ya kujaribu kujiinua kwenye vyeo vya juu katika maisha haya, tunapaswa kuwa
tunafanya nini? Warumi 12:16.
8. Je! Heshima ya kweli itampataje mwaminifu wa Bwana Elohim wetu? 1 Pet. 5: 1-4.
9. Hata ingawa mwanadamu anaweza kuwa katika cheo cha juu na kustawi, je! Inamruhusu kuwa
na kiburi? Zab. 39: 5; 18:27.
10. Je! Uzima wa mtu unahusisha vitu alivyo navyo? Luka 12:15.
11. Je! Nini kitatokea kwamtu aliyeinuliwa na ambaye anajitumainia? Luka 12: 16-21.
******************************
Somo la Januari 25, 2020 (Tevet 28, 5780)
THAWABU YA KUMKUBALI YAHSHUA
Somo Kuu: Mat. 19: 23-30.
Fungu La Kukariri: Mat. 16:27.
1. Je! Thawabu itakuwa gani kwa kuacha yote na kumfuata Yahshua? Mat. 19: 27-29.
2. Ni nini ingine inahitajika ili kupokea thawabu hii? Mat. 10: 37-39.
3. Je! Kazi yetu kwake ni lazima iwe kubwa? Mstari wa 42.
4. Je! Kuna ukomo juu ya kile tunaweza kufanya? 1 Wakor. 3: 6, 7.
5. Ni nani basi mfanyikazi mkuu pamoja nasi? Mstari wa 8 na 9.
6. Ni onyo gani limetolewa kuhusu kazi yetu na Masihi Yahshua? Mstari wa 10.
7. Je! Mtu anapaswa kufikiria kuanza kazi yake kibinafsi? Mstari wa 11.
8. Je! Ni faida gani katika kufanya kazi ikue na kudumu? Mstari wa 13, 14.
9. Je! Ni maonyo gani mengine yaliyopewa katika sura hii kuhusu jinsi tunavyomfanyia kazi?
Mstari wa 18, 19, na 21.
10. Je! Ni ni maneno gani ya kutia moyo ambayo nabii Azaria alimpa Mfalme Asa wakati mmoja?
2 Nya. 15: 1-7.
11. Je! Matokeo ya kufurahisha yalikuwa gani? Mstari wa 8-15.
12. Ni aina gani ya kazi ambayo tunafaa kudumu kufanya, Je! Itakuwa ya bure? 1 Wakor. 15:58.
13. Je! Kuna rekodi mbinguni ya kazi yetu, na sala zetu hapa duniani? Matendo 10: 1-4.
******************************
Somo la Februari 1, 2020 (Shevat 6, 5780)
NGUVU ZA ROHO KATIKA MAISHA
Somo Kuu: Warumi 8: 1-14.
Fungu La Kukariri: Warumi 8:11.
1. Ili kuwa huru kuhukumiwa, watu wa Elohim wanapaswa kuenenda aje? Warumi 8: 1.
2. Jinsi gani tutaweza kuhukumu kwa usahihi na kujua kuwa tunaenenda katika roho? Warumi 8:
4.
3. Je! Malipo yatakuwa gani - ya kidunia na ya milele kwa wale walio na nia ya kiroho? Warumi
8: 6.
4. Je! Kielelezo cha uhakika ya maisha ya mtu ni nini? Mat. 12:34, 37.
5. Je! Ni nini inapaswa kuwa sala ya kila siku kwa kila mtu anayetafuta makao katika Ufalme wa
Elohim? Zab. 19:14.
6. Wakati watu wa Bwana wanapokuwa na nia ya kiroho, mazungumzo yao yatakuwa aje? Zab.
50:23.
7. Je! Inawezekana kumpendeza Elohim tunapokuwa katika njia za asili za kimwili? Warumi 8: 8.
8. Ni nini kinachohitajika kukaa ndani ya kila mwana wa Elohim, ili asiufuate mwili? Warumi 8:
9.
9. Ikiwa roho hii itakaa ndani yetu na kudumu, ni kazi gani ambayo hatimaye itafanyika? Warumi
8:11.
10. Je! Tunawezaje kupata uwepo wa Roho Mtakatifu? Luka 11: 11-13.
11. Je! Ni sifa gani muhimu ya KiMasihi ambayo Roho Mtakatifu huweka ndani ya mioyo yetu?
Warumi 5: 5.
12. Ni kwa njia gani na kwa nguvu gani tutaweza kushinda mwenendo asili wa mwili? Warumi
8:13, 14.
13. Tukiongozwa na Roho, ni wapi tutakuwa tunahifadhi hazina zetu? Mat. 6: 19-21.
******************************
Somo la Februari 8, 2020 (Shevat 13, 5780)
MAISHA YA MITUME
Somo Kuu: Matendo 2.
Fungu La Kukariri: Matendo 2:42.
1. Je! Mtume Petro alisema kuwa wafuasi wa Bwana wanapaswa kutumia mfano wa nani? 1 Petro
2:21; 1 Yohana 2: 6; Waefeso 5: 1.
2. Katika kufuata nyayo za Yahshua, jinsi gani mitume wa Yahshua walikuwa na bidii na shauku;
katika kufuata wito wa mbinguni? Mathayo 4: 18-22; Marko 10:28.
3. Baada ya kuacha shughuli zao za kibinafsi (kazi) kwa sababu ya Injili, Je, wengine wao
walikuwa watumishi na viongozi wakuu wa serikali za nchi yao walitendaje? Luka 5: 27-32;
Wafilipi 3: 7,8; Luka 19: 1-8.
4. Ni kwa njia gani wanafunzi hawa wa Yahshua waliojitolea walipata riziki yao? 1 Wakorintho
4:12; Matendo 18: 3.
5. Je! Kulikuwa na mapatano na umoja wa nia na moyo katikati yao? Matendo 4:32; 2:46.
6. Je! Mitume walikuwa na nia gani kuhusu msiba na ustawi wa ndugu zao? Waefeso 1: 15-19.
7. Walitesekaje kwa sababu ya Yahshua na Injili? Waebrania 11: 36-38.
8. Walikuwa wakarimu kiasi gani? Matendo 2:45; 4:32.
9. Je! Tabia ya maisha yao kwa roho ambazo zilivutwa kwa Bwana kupitia kwa mahubiri yao
ilikuwa ipi? 1 Wathesalonike 2: 2; 5: 7-10.
10. Je! Walikuwa na maoni gani kuhusu mateso na dhiki kwa wale waliowatesa? Matendo 5: 40,41;
2 Wakorintho 12:10.
11. Je! Mathiya alihesabiwaje na mitume kumi na mmoja? Ilikuwa ni kwa upendeleo, uteuzi,
kuonewa, uchaguzi wa kura nyingi au kwa kutupa kura (casting lot)? Matendo 1: 23-26.
12. Walichukuliaje ushirika wa pamoja wa ndugu? Matendo 2: 42-46.
******************************
Somo la Februari 15, 2020 (Shevat 20, 5780)
PETRO – MVUVI WA WANADAMU
Somo Kuu: Yohana 21: 3-17.
Fungu La Kukariri: Mathayo 4:19.
1. Mathayo 4: 18-20 inasimulia juu ya wito wa Simoni Petro na kaka yake Andrea. Je! Yahshua
aliwaita na ahadi gani ya kushangaza? Walijibuje?
2. Linganisha tukio hili na Yohana 1: 35-42.
3. Jadili tukio hilo, tukio ambalo Mathayo 14:28 ni sehemu yake. Je, inadhihirisha tabia ya Petro?
4. Labda sehemu ya utukufu zaidi ya ushirika wa Petro na Yahshua imenakiliwa katika Luka 9:
28-36. Aliichukuliaje? Kwa nini waliiweka siri? Mathayo 17: 9.
5. Ni tukio gani chungu zaidi katika ushirika wake na Yahshua? Mathayo 26: 69-75. Matokeo haya
yalikuwa nini katika maisha ya Petro?
6. Je! Ni nini maagizo ya Masihi kwa Petro? Yohana 21: 15-17.
7. Je! Petro alitii amri hii? Jadili Matendo 2:14, 37-40; 5: 12-16.
8. Je! Ushauri wa Petro katika 2 Petro 3: 11-14 unalingana aje na maisha yake? Ni ushauri mzuri?
******************************
Somo la Februari 22, 2020 (Shevat 27, 5780)
PAULO, MUINJILISTI MKUU
Somo Kuu: Matendo 9: 10-20.
Fungu La Kukariri: 2 Timotheo 4: 7.
1. Je! Ni nini tunajua kuhusu maisha ya awali ya Paulo? Matendo 22: 3. Kamusi ya Bibilia ya
Smith inaonyesha kwamba labda alipelekwa Yerusalemu akiwa kijana kwa ajili ya elimu yake.
Maelezo: Jina Sauli linamaanisha "uliza," tamanika." Jina Paulo linamaanisha" mdogo "au"
chache" majina haya ni sahihi katika maisha ya mtume. Alitamaniwa na wanadamu, mashuhuri
sana na kuaminiwa sana na viongozi. Baada ya kubadilika kwake, hata hivyo, alikuwa
mnyenyekevu sana.
2. Jadili hoja zifuatazo katika tukio la kubadilika kwa Paulo (Matendo 9). Lengo la kwenda
Dameski. Maono ya Sauli. Sehemu ya Anania.
3. Je! Paulo alifanya nini? Kwa nini aliondoka kutoka Dameski? Matendo 9: 22-25.
4. Alipokelewaje huko Yerusalemu, na alienda wapi kutoka huko? Matendo 9: 26-30.
5. Jadili Matendo 11: 19-30; 12: 24-25; 13: 2,3. 6.
6. Je! Walitimiza lengo lao? Warumi 15: 25-28; 1 Wakorintho 16: 1-3; 2 Wakorintho 8: 1-5; 9: 1-
12.
7. Jadili Matendo 20: 22,23; 21: 10,11,33.
Maelezo: Kuanzia siku ambayo unabii wa Agabo ulitimia mnamo A.D. 58, Paulo alikuwa
mfungwa wa utawala wa kirumi hadi mwaka wa 63, wakati huo aliruhusiwa kuishi katika
nyumba yake mwenyewe (Matendo 28:30). Alikamatwa tena mnamo A.D. 65 na kukatwa
kichwa katika A.D. 67 au 68.
8. Je! Una lipi la kusema kuhusu mwenendo wake wakati alipokuwa ameshikwa.
******************************
Somo la Februari 29, 2020 (Adar 4, 5780)
UJUMBE WA MWISHO YA PAULO KWA KANISA
Somo Kuu: 2 Timotheo 4: 1-8.
Fungu La Kukariri: 1 Timotheo 5: 7.
1. Je! Paulo alitoa maelezo yake ya mwisho mbele ya nani, na alisema ni wakati gani walio hai na
wafu watahukumiwa? 2 Timotheo 4: 1.
2. Je! Aliwaambia watu wake wahubiri nini, nanini kuhusu matumizi ya mafundisho? 2 Timotheo
4: 2.
3. Je! Alitoa unabii gani juu ya nia ya watu kuhusu mafundisho yaliyo ya kweli? 2 Timotheo 4: 3.
4. Je! Alisemaje kuhusu watu wa siku za mwisho kwa ujumla wangechukulia ukweli, na
wangegeukia nini? 2 Timotheo 4: 4.
5. Je! Alimuamuru vipi Timotheo kuhusu dhiki juu ya kazi iliyokuwa mbele yake? 2 Timotheo 4:
5.
6. Je! Paulo alikubali hatma yake na alikuwa tayari kufariki? 2 Timotheo 4: 6.
7. Je! Alikuwa ameridhika kabisa na vita vya maisha yake alivyokuwa amepigania sana, na alijua
kuwa ameshinda? 2 Timotheo 4: 7.
Maelezo: Kila mwana wa Elohim anapaswa kuridhika na maisha yake. Anapaswa kujua kila
siku kuwa anapigana vita vizuri vya imani.
8. Ni nini sasa ilikuwa faraja kubwa na tumaini la Paul, na alitarajia na kutazamia kupokea
thawabu yake wakati gani? 2 Timotheo 4: 8 [sehemu ya mwisho].
9. Ni nani aliyesimama na Paul, akimpa nguvu ya kupigana vita vya maisha? 2 Timotheo 4:17.
10. Je! Paulo alikuwa anajali sana juu ya kuokolewa kutoka kwa dhiki au kutoka kwa kazi mbaya?
2 Timotheo 4:18.
11. Katika shauri la mwisho la Paulo kwa Tito, alisema nini juu ya kukataa ubaya na tamaa? Tito
2:12.
12. Je! Ni nini tunapaswa kutazamia kwa furaha na matarajio kila wakati? Tito 2:13; 2 Timotheo 4:
8, [sehemu ya mwisho].
******************************
Somo la Machi 7, 2020 (Adar 11, 5780)
WAKATI WA MWISHO NA UKOMBOZI
Somo Kuu: Zaburi 91.
Fungu La Kukariri: Danieli 12: 1.
1. Kabla tu ya wafu kufufuliwa, ni hali gani zitakua duniani? Danieli 12: 1,2; Ufunuo 11:18.
2. Ni mji gani utafanywa kuwa mzigo kwa mataifa yote; ambao wataelekeza majeshi yao wakati
wa shida? Zekaria 12: 2,3; 14: 1-3.
3. Ni nini hasa imesemwa kuhusu wale ambao ni wenye hekima katika kumjua Elohim wakati wa
mwisho? Danieli 12: 3, 4, 10.
4. Je! Ni nini imesemwa zaidi juu ya walinzi wa Elohim? Isaya 52: 8, 9.
5. Je! Inasemwa nini kuhusu magari ya vita (njia za kisasa za kusafiri), wakati ujumbe wa
maandalizi ya Elohim unaendelea katika siku hizi za mwisho? Nahumu 2: 3, 4.
6. Je! Ni nini kilichotabiriwa kuhusu hali ya mioyo ya wanadamu, na dhiki katika mataifa ya
ulimwengu, kabla ya kuja kwa Bwana? Luka 21: 24-27.
7. Wakati nyakati za shida zinatokea ulimwenguni, mataifa yatakuwa yakifanya nini kujaribu
kuzuia maafa? Isaya 8: 9,10.
8. Je! Ni nini Bwana anasema watu wake wasifanye? Mstari wa 12.
9. Je, tutatazamia msaada wetu kwa nani? Mstari wa 13; Sefania 2: 3.
10. Je! Watu wa Elohim watajali sana ujumbe upi? Isaya 8:16.
11. Je! Watu wa dunia watahukumiwa kwa kiwango gani kikubwa? Mstari wa 20; Ufunuo 12:17;
14:12.
12. Je! Ni nini itatokea kwa mtumwa asiye na faida wakati huo? Mathayo 25:30; Luka 12:46.
13. Je! Hali itakuwa gani katika ulimwengu wote nyakati za Mataifa zinapoisha? Luka 21:26, 27,
34, 35.
14. Ili tuokolewa, tumeamrishwa tufanye nini? Luka 21:36.
******************************
Somo la Machi 14, 2020 (Adar 18, 5780)
UFUFUO
Somo Kuu: 1 Wakor. 15: 1-58.
Fungu La Kukariri: 1 Wakor. 15:22
1. Kila mtu atafufuliwa? Yohana 5:28, 29.
2. Ni lini watakatifu watafufuliwa kwa uzima wa milele? 1 Wakorintho 15:22-23; Ufunuo 20:4-6;
1 Wathe 4:16.
3. Je, ni nini kitatokea kwa watakatifu ambao watakuwa hai katika kuonekana kwa Yahshua? 1
Wathe 4:17; 1 Wakorintho 15:51-53.
4. Ni wapi ambapo watakatifu watakaofufuka watakaa, na nini itakuwa kazi yao wakati wa
milenia?Ufunuo 5:10; Danieli 7:27.
Maelezo. Ni baraka za ajabu gani watapata waamini wote katika Masihi Yahshua! Wote
waliokufa katika Bwana watahuishwa katika kuonekana kwa Yahshua, watakatifu walio hai
watabadilishwa katika dakika moja, kufumba na kufumbua, wataishi na kutawala pamoja na
Masihi kwa miaka elfu. Wakati huu Yahshua atakuwa akitawala katika kiti cha enzi cha Daudi.
5. Je, wafu waovu watakuwa wapi wakati wa utawala wa miaka elfu wa Bwana Yahshua? Ufunuo
20: 5, 6.
6. Je waovu wataifufuliwa? Yohana 5:28, 29.
7. Ni kwa madhumuni gani waovu watafufuliwa? 2 Petro 2:9.
8. Wakati waovu watafufuliwa ni wapi ambapo wataonekana? Ufunuo 20:11-13.
Maelezo. Hukumu ni kwa ajili ya waovu, kwa vile wenye haki walienda katika hukumu wakati
walikiri dhambi zao, wakazaliwa tena na wakawa watiifu kwa neno la Bwana; hivyo wao
walipita kutoka mautini kuingia uzimani na wakawa washiriki wa familia ya Elohim. 1Tim
5:24, Yohana 5:24.
9. Je, hatima ya waovu itakuwa ipi? Ufunuo 20:13-15, 21:8
******************************
Somo la Machi 21, 2020 (Adar 25, 5780)
SABATO NI SIKU GANI?
Somo Kuu: Waebrania 4: 1-16.
Fungu La Kukariri: Yer. 17: 21-22.
1. Je! Tunaweza kujua Sabato ni siku gani? Mat. 28: 1.
2. Je! Musa alijua ni siku gani ilikuwa Sabato kabla haijapeanwa katika Mlima Sinai? Kutoka. 16:
23-25.
3. Je! Siku ya Sabato ilipaswa kutunzwa kwa muda gani? Kutoka 31:16, 17.
Maelezo: Milele inamaanisha pasipo mwisho; hakuna mwisho wake.
4. Je! Siku ya Sabato itatunzwa katika utawala wa miaka elfu wa Mwokozi? Isa. 66:23.
5. Je! Ni ishara gani kwa watu kudhibitisha kuwa wametakaswa (wamewekwa wakfu)? Ezekieli.
20:12, 20; Kutoka. 31:13, 14.
6. Mwokozi alisema nini kuhusu Sabato? Ilikuwa imewekwa tu kwa Wayahudi, au ni kwa watu
wote? Marko 2:27.
7. Je! Mwokozi aliiheshimu siku ya Sabato? Mat. 24:20; Luka 4: 16-18.
Maelezo: Yerusalemu iliharibiwa katika mwaka wa 70A.D., na hakutaka kukimbia kwao kuwe
siku hiyo.
8. Je! Wanawake watakatifu waliitunza siku ya Sabato baada ya Mwokozi kuwekwa kaburini?
Luka 23: 55-56.
9. Je! Paulo aliitunza siku ya Sabato, na kusema bado ingali? Matendo 13: 42-44, 16: 13- 13, 18:
1-4; Waebrania 4: 9.
10. Je! Watu waliuawa kwa kufanya kazi siku ya Sabato? Hesabu 15: 32-36.
Maelezo: Sabato bado ni takatifu na ni sheria leo kama ilivyokuwa siku zote, na ni kitendo cha
kutotii kuinajisi. Tumepewa siku sita kwa kazi zetu, lakini Sabato ni siku ya Bwana, na sio mali
yetu. Hatuna haki ya kuitamani, au kuiiba, na kuitumia kwa kazi zetu wenyewe na biashara.
******************************
Somo la Machi 28, 2020 (Nisan 3, 5780)
CHANZO NA UMUHUMI WA UNABII WA BIBILIA
Somo Kuu: 2 Petro 1: 1-21.
Fungu La Kukariri: 2 Petro 1:21.
1. Je! Maandiko yote yamepeanwa aje? 2 Timotheo 3:16.
2. Yamepeanwa kwakusudi gani? 2 Timotheo 3:17.
3. Je! Unabii huu ni wetu wakati wa leo? Na utafanya nini? Kumbukumbu la Torati 29:29.
4. Je! Kitabu cha mwisho katika Bibilia kinaitwaje? Ufunuo 1: 1.
5. Je! Bwana Elohim aliwaahidi nini wale wanaosoma unabii huu? Ufunuo 1: 3.
6. Unabii wa Agano la Kale ulipeanwa aje? 2 Petro 1:21.
7. Je! Ni nini imesemekana kuhusu tafsiri wa huu unabii? 2 Petro 1:20.
8. Je! Roho wa Masihi alikuwa na uhusiano wowote na manabii? 1 Petro 1:11.
9. Kuja kwa Masihi kulifunuliwaje kwake Petro? 1 Petro 1:11, 12.
10. Je! Unabii huu ni nini kwetu katika siku za leo? 2 Petro 1:19; 1 Wakorintho 10:11; Warumi 15:
4.
11. Je! Mtu wa kweli aliyechaguliwa, aliyeitwa na Baba wa Mbingu kwa uzima wa milele, atakuwa
mwenye kuzaa au asiyezaa matunda katika kazi ya Bwana wakati huu? 2 Petro 1: 8.
******************************
© 2012 Church of Elohim 7th Day ~ Powered by Kenesiyahmessenger ~ Powered by wix